CHAMA CHA MAPINDUZI
UMOJA NI USHINDI, AMANI NA MAENDELEO ...!!!

Tuesday, April 8, 2014

RIDHIWANI KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO JIMBONI CHALINZE

Ngd. Ridhiwani Kikwete
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Ngd. Ridhiwani Kikwete ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani.

Katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Aprili 6, 2014, CCM imepata ushindi wa asilimia 86.53 ikiwa ni sawasawa na kura 20,812. Vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo ni pamoja na Chadema waliopata asilimia 10.92 ambayo ni sawasawa na kura 2,628, CUF wamepata asilimia 1.92 sawasawa na kura 473. APF kimepata asilimia 0.32 sawasawa na kura 78, huku NRA kimepata asilimia 0.24 sawasawa na kura 59.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Marehemu Saidi Bwanamdogo, ambaye alifariki Januari mwaka huu.


Wednesday, April 2, 2014

RIDHIWANI AENDELEA NA KAMPENI YA UBUNGE KATIKA KIJIJI CHA TOKAMISASA, JIMBONI CHALINZE

Mgombea ubunge katika jimbo la Chalinze
kwa tiketi ya CCM
Ndg. Ridhiwani Kikwete.
  • Jana , Aprili 1, 2014, Ndg. Ridhiwani aliendelea na kampeni yake ya kujinadi kwa wananchi wa kijiji cha Tokamisasa, jimboni Chalinze.
  • Awaahidi wananchi wa Tokamisasa kuwa ataanza na Barabara, kisha elimu, afya pamoja na kurudisha michezo jimboni humo.
  • Pia awaahidi kuhakikisha anamaliza tatizo la mgogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi kijijini hapo.

Ndg.Ridhiwani Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Tokamisasa wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge zinazoendelea jimboni Chalinze.
Ndg. Ridhiwani akihutubia wakazi wa kijiji cha Tokamisasa.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza muziki na Miraji Mtaturu, Katibu wa CCM  Wilaya ya Mufindi wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze uliofanyika kwenye kitongoji cha Mbuyu kijiji cha Tokamisasa kata ya Ubena Zomozi.
Msanii Sam wa Ukweli akitumbuiza kwenye kampeni za CCM zilizofanyika katika kijiji cha Tokamisasa kitongoji cha Mbuyu.
Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wazee wa kijiji cha Tokamisasa wakati akiwasili kwenye kitongoji cha Tuka Mjini tayari kwa kufanya mkutano wa kampeni.
Msanii wa Mashairi Mwanahamisi Mohamed wenye ulemavu wa macho akiimba shairi linaloitwa Changamoto wakati wa mkutano wa CCM wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze.
Wakina Mama wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za ubunge za CCM ambapo Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mgombea ubunge kwa tiketi ya  CCM ) alifika katika tawi la Kivuga na kuomba kura.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi - CCM, Ndg.Nape Nnauye akizungumza na wafugaji wa Kimasai wa Tawi la Kivuga kata ya Ubena Zomozi wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze.
Ndg. Ridhiwani Kikwete akizungumza na vijana wajasiriamali wa UVCCM mshikamano Visakazi mara baada ya kuzindua shina hilo lililopo katika kata ya Ubena Zomozi.
Ndg. Ridhiwani akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Tokamisasa, kata ya Ubena Zomoni wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana Aprili 1, 2014 jimboni Chalinze.
Mgombea ubunge katika jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ndg. Ridhiwani Kikwete akishiriki kucheza mziki na wananchi wa kitongoji cha Mbuyu, katika kijiji cha Tokamisasa, kata ya Ubena Zomoni, wakati wa muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za ubunge iliyofanyika jana Aprili 1, 2014.

 

Tuesday, April 1, 2014

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI NKASI, MKOANI RUKWA


Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wake kuhusiana na hatua za awali za ujenzi wa bandari ya Kabwe, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.
Mmiliki wa Kampuni ndogo ya kusindika samaki Bw. Nassor Shibib akimpa maelezo mafupi Ndg. Kinana kuhusu namna ya kuhifadhi samaki aina ya migebuka kabla ya kusafirishwa na wafanyabiashara wa eneo hilo na kuuzwa katika nchi za Zambia, Congo, Burundi na Rwanda.
Ndg. Kinana akipata maelezo mbalimbali kuhusiana na suala la uvuvi katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kujengwa bandari.
Ndg. Kinana akiangalia samaki aina ya migebuka katika kiwanda kidogo cha kuhifadhia samaki hao, kijijini Kabwe katika wilaya ya Nkasi.
Samaki aina ya migebuka ikiwa imeandaliwa kwaajili ya kukaushwa kabla ya kuhifadhiwa kwenye majokofu na kusafirishwa maeneo mbalimbali, ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Mhe. Ally Keisy alipokwenda kukagua ujenzi wa bandari ya Kabwe ambao uko katika hatua za awali, na kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi zinazofanyika katika kijiji hicho cha Kabwe.
Ndg. Kinana akishiriki katika ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kabwe, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.
Ndg. Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM, jana , katika kijiji cha Kabwe, wilayani Nkasi. Aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali inatambua matatizo yao likiwemo suala la pembejeo za kilimo, maji pamoja na uvamizi wa wavuvi.
"Miradi yote inayotekelezwa nchi nzima kwa sasa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010, hatubagui kwa kuwa wote ni watanzania ..." alisema Ndg.Kinana. Pia aliongeza kuwa Serikali inatambua vizur kuwa shughuli kubwa kijijini hapo ni uvuvi, hivyo itajitahidi kuwe na utaratibu wa kuwasaidia kupata mikopo ili waweze kununua zana za uvuvi kusudi waweze kujiendeleza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kirando, wilayani Nkasi mapema jana. Ndg. Kinana alisema kuwa atahakikisha barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda kijiji cha kwabwe inatengenezwa kwa kiwango cha lami. "Nitaenda kwa mbunge wenu kushinikiza suala la barabara jii ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia shughuli za kibiashara ..." alisema. Pia aliongeza kuwa ... maendeleo hayawezi kuja ikiwa miunombinu ni mibovu hivyo, atahakikisha analifikisha suala hilo kwa waziri mwenye dhamana pamoja na mkuu wa nchi ili kazi hiyo ifanyike mapema.


Monday, March 31, 2014

RIDHIWANI AENDELEA NA KAMPENI YAKE YA UBUNGE KATIKA KIJIJI CHA MKANGE, JIMBONI CHALINZE

Jana Machi 30, 2014, mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Ndg. Ridhiwani Kikwete aliendelea na kampeni yake ya kuomba ridhaa ya wananchi waishio katika kijiji cha Mkange, katika jimbo la uchaguzi la Chalinze, ili wamchague kuwa mbunge wao.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Dini kwenye Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange wakati alipopita kuwasalimia na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Jana Machi 30,2014.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Sam wa Ukweli akitoa Burudani kwa wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Shangwe kwa wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange.
Wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana kwa furaha na wakinamama wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini Mzee Hussein Mwindadi ambaye ni Baba wa Diwani wa Kata ya Mkange.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitaniana na Mzee Nassor Samnamwanja wa Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Wakazi wa Kijiji cha Manda Mazingara wakiwa wameshika mabango ya Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati walipokuwa wakimkaribisha Kijijini kwao.
Kikundi cha Kwaya ya Kijiji cha Manda Mazingara kikitoa Burudani.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Manda Mazingara,Ibrahim Rajab Mahede akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya Kijiji kwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Diwani wa Kata ya Mkange,Abdallah Mwendadi , Ndg. Ridhiwani Kikwete pamoja na wananchi wengine wakisikiliza jambo kwa makini.
Diwani wa Kata ya Mkange,Abdallah Mwendadi akiwasalimia wananchi wake wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM katika Kijiji cha Manda Mazingara jana Machi 30,2014.
Meneja wa Kampeni wa CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Manda Mazingara jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Manda Mazingara wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsalimia Mzee Salum Ramadhan Satajiri.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akionyeshwa maendeleo ua ujenzi wa Msikiti (haupo pichani) na Sheikh Yahya Abdullah Imam wa Msikiti huo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza machache na wananchi wa kijiji cha Chamakuru,aliposimama kuwasalimia akiwa safarini kwenye Kijiji cha Miono.
Wananchi wa Kijiji cha Manda Mazinga wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika jana Machi 30,2014.